
Ikiwa wewe au mtu mwingine yupo hatarini mara moja, piga polisi kwa Tatu Sufuri (000).
Ikiwa unaamini mtoto yupo hatarini, unaweza kuripoti wasiwasi wako kwa Idara katika Jimbo au Wilaya yako.
Utambulisho wa aliyefanya ripoti kwa kawaida unashikwa siri.
Sheria kuhusu lini watu wanapaswa kuripoti watoto hatarini kwa Idara ni tofauti kidogo katika kila Jimbo na Wilaya. Ili ujue zaidi jinsi na lini ya kuripoti, tembelea wavuti wa Idara ya ulinzi wa watoto ya eneo lako.